Wanachuo
wa chuo cha sanaa bagamoyo wakicheza ngoma kwenye tamasha la sanaa la
kimataifa linalofanyika katika viwanja vya chuo cha sanaa bagamoyo
wakionyesha umahili wao wa kuisakata ngoma .mbele ya mgeni rasimi
katika ukumbi wa chuo bagamoyo mkoani pwani
Watoto
wadogo Gozibet Bwere miaka minne na mwingine Nyambuli Aginess Muganga wa
kikundi cha ngoma cha Utandawazi Theater Group Matwigachallo, kutoka
kijiji cha Nansore Wilaya ya ukerewe mkoa wa mwanza wakiwa wanacheza
ngoma katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamo kwenye Tamasha la
kimataifa la 32 la sanaa na Utamaduni Bagamoyo, kauli mbiu ni sanaa na
utamaduni katika kukuza Utalii.
Msanii
maarufu hapa nchi wa muziki wa kisasa Misoji Nkwambi wa katikati, wa
kushoto ni mwanachuo Safina Amani na wakulia ni Clement Chares akicheza
ngoma na hivi sasa Misoji ni mwanachuo wa chuo cha sanaa bagamoyo.(hd)
NAIBU WAZIRI AMOSI MAKALA; " Sanaa na utamaduni kuleta ajira"
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
NAIBU
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala amesma Sanaa
na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta ajira vijana pindi
watakapokuwa tayari kuienzi kwa vitendo na kuisomea.
Makala
alisema hayo mjini hapa alipokuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa tamasha
la 32, la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lenye kauli mbiu 'Sanaa na
Utamaduni katika kukuza utalii' linaloshirikisha vikundi zaidi ya 70,
kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Akihutubia,
umati wa wananchi,wanafunzi wa chuo hicho cha sanaa na vikundi
mbalimbali vinavyoshiriki, Waaziri Makala alisema akiwa waziri mwenye
dhamana atahakikisha utamaduni na sanaa nchini inakua huku ikiwanufaisha
watu wote kwa vizazi vya sasa na vya baadae.
"Katika
kuenzi Sanaa na Utamaduni, Wizara ina mipangilio mingi ikiwemo nay a
kuakikisha tunakuza utamaduni wa Taifa letu na hata ajira kwa vijana
ambao watajiunga na sanaa hivyo tutaendelea kushirikiana na chuo cha
TasuBa na wadau wengine katika kufikia malengo" alisema Makala.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Michael Kadinde alisema
watahakikisha tamasha hilo kongwe nchini wanafikia vikundi na wasanii
mbalimbali ilikupata kushiriki na kuonesha kazi zao.
"Lengo
kufikia wasanii wote na hilo tunafanya kila mwaka na zaidi milango ipo
wazi kwa mashirika binafsi ya ndani na nje kuja kuwekeza na kukuza sanaa
zetu" alisema Kadinde
Na
kuongeza kuwa kwa sasa TaSUBa ina enzi na kulithisha sanaa na utamaduni
kwa vitendo ikiwemo kutoa mafunzo kwa watoto wadogo na wale wa elimu ya
msingi.
..
Kwa upande wa Vikundi vinavyoshiriki kwenye tamasha hilo ni pamoja na ;
Alisema,
vikundi 40 kati ya 60, ni kutoka Tanzania na vingine ni kutoka nje ya
nchi vikiwemo vilivyowahi kushiriki tamasha hilo na vipya ambavyo
itakuwa ni mara ya kwanza kuja.
Alivitaja
vikundi vya Tanzania kuwa ni Ngome International Magic Show – JWTZ,
Splendid Theatre, Kigamboni Community Centre, Malezi Youth Theatre na
Jivunie Tanzania Sanaa.
Vingine
ni Mapoloni Culture Centre, Albino Revolutionary, Cocodo African Music,
Imani Theatre, Safi Theatre, Imara Boma, Bagamoyo House of Talents,
Bwagamoyo Africulture, Godykaozya & Tongwa Band na Mtoto Mchoraji.
Vimo pia
Shada Acrobatics, Bagamoyo Players, Bayoice, Jikhoman & Afrika Sana
Band, Vitalis Maembe & The Spirit Band na Bagamoyo Dance Company.
Aidha,
kuna vikundi vya Makini Organization (Arusha), Tumaini Group (Manyara),
Kimanzichana Vijana Group (Mkuranga), Utandawazi Theatre Group (Matwi
Gha Chalo), kutoka visiwa vya Ukerewe, Hiari ya Moyo (Dodoma), Moshi
Police Academy (Moshi), CBM Acrobatic Group, Man Kifimbo Band na Midundo
ya Sanaa. Pia kuna vikundi kutoka Ethiopia , Kenya , Norway , Uganda ,
Rwanda na Ujerumani.
No comments:
Post a Comment