
Hizi
ni picha za jinsi semina ya fursa ilivyoenda leo 28/9 mchana. Kulikuwa
na wazungumzaji mbalimbali kama Lulu,Mr Sebastian Maganga,Mr Ruge
Mutahaba, Nikki wa Pili na wengine wengi.
Cheki jinsi watu wangu wa
Mwanza walivyopata darasa la fursa na baadaye show ya Fiesta inafanyika
ndani ya CCM Kirumba

Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha
akizungumza fursa mbalimbali zipatikanazo na Benki ya Wanawake,ikiwemo
na kutoa mikopo kwa wajasiliamali.

Mrisho Mpoto kama kawaida yake bila viatu lakini anatoa darasa zito

Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akizungumza mada
iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini.

Naibu
Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akimtambulisha mmiliki wa
hotel kubwa ya kitalii hapa jijini Mwanza, Gold Crest,Bwa.Mathias
Erasto,ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini

Mkuu
wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida,Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada
yake iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake

Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akizungumza

Mmoja wa wasanii wa hiphop,Nikki Wa Pili akizungumza kwenye semina ya kamata fursa twenzetu.

Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Maxcom inayouza bidhaa yake ijulikanayo kama Max
Malipo,Bwa.Juma Rajab akizungumzia kuhusiana na fursa ya bidhaa yake ya
Max Malipo inavyoweza kuisadia jamii kwa namna moja ama nyingine.

Picha na michuzijr.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment