Thursday 14 November 2013

Nay wa Mitego kuachia wimbo mpya 'Nakula Ujana' tarehe 20

 Nay wa Mitego akiwa studio        




               
Hitmaker wa Salam Zao 'Nay wa Mitego' anatarajia kuachia wimbo mpya 'Nakula Ujana' kwania ya kuwaonyesha watu kwamba habahatishi kwenye game
.

Akizungumza na tovuti hii alisema kumekuwa na maneno mengi sana kuhusu muziki wake kwamba huwa anabahatisha kila wimbo anaoufanya kwa hiyo basi tarehe 20 atadondosha kitu cha tofauti kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva.

'Kume kuwa na maneno mengi kwamba mimi nabahatisha kwenye huu muziki sasa basi nataka niwahakikishie kwamba tarehe 20 nitaachia wimbo wangu mpya 'Nakula Ujana' ni wimbo wa tofauti kabisa nadhani shabiki akiusikiliza atanielewa,mara nyingi sibahatishi kazi zangu'Alisema Nay wa Mitego
www.thefame.blogspot.com

No comments:

Post a Comment