Wednesday, 2 October 2013

VODACOM KUUNGA MKONO JITIHADA ZA WAUGUZI KUFIKIA MALENGO YA MILLENIA

Meneja Uendelezaji Biashara wa Vodacom Tanzania Bw. Moses Krom akiwaonesha tisheti Wajumbe wa Chama cha Wauguzi Tanzania (Hawapo pichani) zilizotolewa na kampuni hiyo katika mkutano Mkuu wa 41 wa Chama hicho uliofanyika mkoani Tabora,

Kampuni hiyo imeahidi kuunga mkono jitihada za wauguzi katika kufikia Malengo ya Millenia na 4, 5 na 6.





Baadhi ya wajumbe na wageni waalikwa katika Mkutano Mkuu wa 41 wa Chama Cha Wauguzi Tanzania wakisikiliza mada mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa Chama hicho, Pamoja nao katika picha ni Meneja Uendelezaji Biashara wa Vodacom Tanzania Bw. Moses Krom.(P.T)


Msaada tafadhal sana


TABORA 2 Sep 2013. . Katibu Mkuu Mwenezi wa Chama cha Wauguzi Tanzania Bi. Daflosa Mzava, ametoa wito kwa wadau mbalimbali wanaopenda maendeleo katika sekta ya afya kujitokeza kusaidia chama hicho katika kuwawezesha kufikia malengo ya milenia namba 4, 5 na 6 yanayolenga kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 na kuboresha huduma za afya ya uzazi.


Akizungumza katika mkutano Mkuu wa 41 wa chama hicho uliofanyika Mkoani Tabora kwa muda wa siku tatu na ukiwa na wajumbe zaidi ya 1000 kutoka Tanzania bara chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania , Bi Mzava alitoa pongezi kwa kampuni ya Vodacom kwa kuwaunga mkono katika kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo huku akitoa wito kwa kampuni nyingine kuiga mfano wa kampuni hiyo na kujitokeza kuisaidia jamii inayowazunguka.


"Kazi tunazozifanya zinakabiliwa na changamoto nyingi sana, sasa tunaangalia namna ambavyo tunaweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufikia malengo ya Milienia namba 4, 5 na sita ili kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 na kuboresha huduma za afya ya uzazi," alisema Bi Mzava na kuongeza,


"Vodacom imekuwa na maamuzi bora na chanya kwa kushirikiana nasi katika masuala haya ya msingi, tunahitaji kutoa huduma bora na zenye usawa kwa wote na ili kufikia malengo haya tunahitaji kupata ushirikiano kutoka kwa wadau kama hawa na wengineo, Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wadau wa sekta mbalimbali watuunge mkono ili kuweza kufikia malengo haya na kuleta tija katika huduma za afya nchini,"


Kwa upande wake, Meneja uendelezaji biashara wa Vodacom Tanzania Bw.Moses Krom amesema Vodacom imeamua kukisaidia chama hicho katika kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya na kupunguza maambukizi ya ukimwi,malaria na magonjwa mengine.


"Tunatambua huduma za afya zinakabiliwa na changamoto mbalimbali, Tumekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha tunarahisisha huduma za afya kwa Watanzania zinakuwa rahisi na bora zaidi, Tumeingia ubia na wadau mbalimbali katika sekta ya afya katika kukabiliana na changamoto hizo" alisema Krom na kuongeza,"Tunaangalia namna sasa ya kuwaunga mkono hawa ndugu zetu wa Chama cha wauguzi ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuokoa maisha ya mamia ya watanzania, Kwa kutumia miundombinu tulionayo kama M PESA tunaamini tunaweza kufikia malengo hayo na kuwa chachu ya huduma bora za afya kwa jamii ya Watanzania."

Mkutano huo uliofanyika kwa siku tatu na kuhitimishwa mwishoni mwa wiki ulijadili masuala mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabili sekta ya afya na namna ambavyo wanaweza kukabiliana nazo huku idadi ya watu inayoongezeka kwa kasi, malipo duni na vifo vya watoto chini ya miaka mitano na miundombinu ya utoaji wa huduma za afya bado zimeendelea kuwa changamoto kuu.

Mwisho...


www.thefameshow.blogspot.com

No comments:

Post a Comment